Answers are grounded in this paper and cite their sources.
Makala hii inachunguza mabadiliko ya kimofolojia ya vitenzi vya Kiswahili katika matini zilizochapishwa kati ya mwaka 1870 na 1970 ili kubainisha mabadiliko ya viambishi vya kabla na baada ya mzizi. Utafiti ulitumia mkabala wa kitaamuli na uchanganuzi wa matini. Matoleo ya magazeti tisa yaliteuliwa kwa usampulishaji nasibu tabakishi; Orodha ya Msamiati ya Steere (1870) pia ilitumika. Vitenzi 68 vilinakiliwa, vikalinganishwa na maumbo ya Kiswahili sanifu na kuchanganuliwa kwa kuongozwa na Nadharia ya Mofolojia Leksika ya Kiparsky (1982). Matokeo yanaonesha mabadiliko katika viambishi vya kiima, njeo, yambwa, urejeshi na viambishi tamati. Mabadiliko hayo yanajumuisha {twa-}, {mwa-} na {wa-} kuwa {tu-}, {m-} na {u-}; kuimarika kwa {-na-} ya wakati uliopo; kubadilika kwa {mw-} kuwa {mu-} mbele ya /u/; kufinyika kwa matumizi ya {-eni} na {-ni}. Makala inahitimisha kuwa mabadiliko hayo yanaakisi upangaji upya, urahisishaji na usanifishaji wa mfumo wa kimofolojia wa vitenzi. Inapendekeza kuundwa kwa korpasi ya matini za kihistoria na kufanyika kwa tafiti kuhusu mabadiliko katika viwango vya lugha na lugha nyingine za Kibantu.
No takes yet. Share an insight, caveat, or question.
Mlowezi et al. (2026) studied this question.
Synapse has enriched 8 closely related papers on similar clinical questions. Consider them for comparative context: