Answers are grounded in this paper and cite their sources.
Makala hii inachunguza wahusika wanawake kama nyenzo kuu ambayo Said Ahmed Mohamed Khamis ametumia kuwasilisha maudhui ya uwezeshaji wanawake katika riwaya tano teule: Asali Chungu (Mohammed, 1977), Utengano (Mohammed,1980), Tata za Asumini (Mohammed,1990), Nyuso za Mwanamke (Mohammed, 2010) na Kamwe si Mbali Tena (Mohammed, 2014). Makala inabainisha idadi na mgawanyiko wa wahusika wa kike katika riwaya hizo, inawaainisha kimuundo kwa uainishaji wa Wamitila (2008) wa wahusika wakuu, wahusika wasaidizi na wahusika wajenzi, na inafafanua mchango wa kila kundi kwa mihimili mitatu ya uwezeshaji ya Kabeer (1999). Utafiti ulikuwa wa kifani na kimseto uliofanywa maktabani, ambapo data zilikusanywa kwa usomaji wa kina na unukuzi wa matini, zikachanganuliwa na kuwasilishwa kimaelezo pamoja na matumizi ya takwimu rahisi katika majedwali. Matokeo yanaonyesha kuwa riwaya teule zina wahusika wanawake sabini na tano na kwamba kuna mgawanyo bayana wa kazi za kimaudhui. Wahusika wakuu wamebeba safari ya uwezeshaji kama mchakato, wahusika wasaidizi wamebeba utetezi wa wanawake wengine, nao wahusika wajenzi wamewakilisha hali halisi ya jamii inayohalalisha uwezeshaji. Mhusika anayeshindwa na mfumo, kama Asumini katika Tata za Asumini (Mohammed, 1990), naye ametumika kama kauli ya kimada dhidi ya ukandamizaji. Makala inahitimisha kuwa wingi na mgawanyo wa wahusika hawa ni uwekezaji wa makusudi wa mwandishi katika sauti za kike.
No takes yet. Share an insight, caveat, or question.
Jenipher Dinah Ondiso (2026) studied this question.
Synapse has enriched 8 closely related papers on similar clinical questions. Consider them for comparative context: